Klabu ya Real Sociedad, imemfukuza kazi kocha wake Eusebio Sacristan, baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa muda miaka miwili na nusu.

Eusebio amefukuzwa mwisho wa wiki iliyopita kufuatia kupoteza mchezo dhidi ya Getafe nyumbani kwa bao 2-1 na kuiacha Real Sociedad katika nafasi ya 15, na pointi 33 baada ya kucheza michezo 29 ikiwa ni nafasi mbaya kukamata klabu hiyo tangu  msimu wa mwaka 2011-2012.

Aidha, Kocha huyo wa zamani wa kikosi cha pili cha Barcelona alijiunga na klabu hiyo kuchukua nafasi ya David Moyes, Novemba 2015, na kuisimamia kwa michezo 112, huku msimu uliopita akiiongoza timu hiyo kufunzu mashindano ya kombe la shirikisho barani ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya sita kwenye ligi ya Hispania,La liga.

Wakati huo huo,Klabu hiyo imemtangaza kocha wa kikosi cha pili Imanol Alguacil kuwa kocha wa muda ambaye ataifundisha Sociedad mpaka mwisho wa msimu.

 

Mama Uwoya asema haitambui ndoa ya mwanae na Dogo Janja.
Promota atabiri Anthony Joshua kupigwa kwa mara ya kwanza