Mwimbaji wa THT, Recho amefunguka kuhusu tuhuma za kutumia dawa za kulevya zilizoelekezwa kwake na baadhi ya watu.

Miss ‘Kizunguzungu’ ameiambia Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa hajawahi kutumia dawa za kulevya katika maisha yake. Amedai kuwa huenda tuhuma hizo zinaelekezwa kwake kwa sababu watu wanamfananisha na Ray C ambaye aliwahi kuwa muathirika wa dawa hizo.

“Kiukweli mimi situmii dawa za kulevya hata kidogo,” alifunguka. “Huwa naumia sana ninapoambiwa taarifa hizi, sijui hata ladha yake, ila nadhani watu wamekuwa wakinifananisha na Ray C, labda ndio sababu ya kuwapo kwa taarifa hizi mitaani.”

Tetesi hizo ziliibuka baada ya kuwepo tetesi za awali kuwa mwimbaji huyo ana uhusiano wa mapenzi na Top In Dar (TID) ambaye pia amekuwa akihusishwa na tuhuma za matumizi ya dawa hizo.

Serena Ajiwekea Rekodi Wimbledon Championship
Wakenya Hati-Hati Kushiriki Kageme CUP
Tags