Kikosi cha Chelsea kitakosa huduma ya wachezaji wake wawili muhimu Reece James na Mason Mount, ambao hawataonekana tena katika mapambano ya Ligi Kuu hadi msimu ujao wa 2023/24.

Chelsea msimu huu imekuwa ikisuasua na haina dalili ya kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao kwani mpaka sasa wapo nafasi 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.

James amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Chelsea japo amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara.

Kuumia kwa James na Mount ni pigo kwani Chelsea kwa sasa imekuwa ikipita katika kipindi kigumu kutokana na aina ya matokeo mabaya inayopata.

Meneja wa muda wa kikosi hicho, Frank Lampard amesema kukosekana kwa nyota hao itakuwa pigo.

Lampard amesema: “Reece James ameumia na kwa jinsi hali ilivyo atakuwa nje mpaka msimu ujao.

“Lakini kwa Mason Mount yeye anaweza kupatikana katika mchezo wa mwisho wa msimu huu japo kwa sasa atakuwa nje.”

Nasredinne Nabi: Hatujafuzu Nusu Fainali
Tanzania mwenyeji mkutano wa Mawaziri Afrika