Wakati kumbukumbu za kitabu cha Guinness kikionesha kuwa raia wa Japan, Yasutaro Koide mwenye umri wa miaka 112 ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani anayeishi, wiki hii mtu mwenye umri mkubwa zaidi yake amebainika nchini Brazil.

Kabla hujafahamu umri wa mtu huyo, nikukumbushe kuwa kitabu cha Guinness kinaonesha kuwa Bibi. Jeanne Calment, raia wa Ufaransa aliyekufa akiwa na umri wa miaka 122 mwaka 1997, ndiye mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani.

Watumishi wa umma Kaskazini mwa Brazili, wameeleza kubaini uwepo wa mzee OAP Joao Coelho de Souza akiwa na cheti chake cha kuzaliwa kinachoonesha amezaliwa mwaka Machi 10 mwaka 1884. Hivyo, mzee huyo ana umri wa miaka 131.

Cheti mtu mzee

Mzee huyo anaishi na mke wake mwenye umri wa miaka 69 pamoja na watoto wake watatu wanaoishi.

Binti yake aliyejitambulisha kwa jina la Cirlene Souza mwenye umri wa miaka 30, aliliambia ‘Daily Records’ kuwa alizaliwa wakati baba yake akiwa na umri wa miaka 101.

Mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani

“Ana siku ambazo anakuwa vizuri, lakini kuna siku ambazo hawezi hata kuwatambua watoto wake,” alisema binti yake. “ameishi na mama kwa zaidi ya miaka 40 na amekuwa akitegemea watu wengine kwa kila kitu,” aliongeza.

Magaidi Waishambulia Indonesia, saba wapoteza maisha
Mohamed Naser Elsayed Elneny Atua Emirates Stadium