Mark Clattenburg ameteuliwa kuchezesha Manchester Derby.¬†Ameshachezesha mara nne dabi hii na kutoa kadi 19 za njano na nyekundu moja. Hiyo nyekundu aliitoa kwa Johnny Evans kwenye mchezo wa 6-1 Old Trafford 2011, unaofahamika zaidi kama “why always me” kutokana na ujumbe wa Mario Balotelli.

Baada ya mchezo huo, meneja wa United, Sir Alex Ferguson, alimlaumu Clattenburg kwa kutoa kadi hiyo nyekundu.

Wakati huo, Ferguson alikuwa na sauti kubwa sana kwenye maamuzi muhimu. Refa yoyote aliyelaumiwa na Ferguson alikuwa hapewi tena mechi za Man U mpaka mwaka mmoja upite na wengine walikuwa wanateremshwa madaraja. Baada ya hapo, wakipewa mechi ya United, lazima wamfurahishe babu.

Clattenburg naye hakupewa tena mechi ya United mpaka mwaka ukapita…mechi yake ya kwanza baada ya ‘adhabu hiyo’ ikawa dhidi ya Chelsea darajani 2012.

Mechi hiyo ilishuhudia wachezaji wawili wa Chelsea, Fernando Torres na Branislav Ivanovic, wakipewa kadi nyekundu huku United wakipewa bao la offside lililofungwa na Chicharito.

United walishinda 3-2 na kuwafanya wapate ushindi wa kwanza darajani kwenye Ligi Kuu tangu 2002.

Ukitaka kupata ‘uchafu’ wa Ferguson na ‘mipango mipango’ yake kwenye EPL, tembelea

Video: Serikali kuanza ujenzi nyumba za wakazi wa Magomeni Kota
Ilkay Gundogan Afikiriwa Kucheza Dhidi Ya Man Utd