Hazijawahi kukutana katika mashindano yoyote zaidi ya CECAFA Senior Challenge Cup tangu yakiitwa Gossage Cup.

Tanzania bara wakati huo ikiitwa Tanganyika ilianza kushiriki Gossage Cup mwaka 1945. Zanzibar ikafuatia miaka miwili baadaye, 1947.

Timu hizi zimekutana mara 35. Tanzania bara imeshinda mara 23, Zanzibar imeshinda mara 9 na mara tatu zimetoka sare.

18- 9-1947
Tanganyika 3-1 Zanzibar – Nusu fainali

10-10-1950
Tanganyika 4-0 Zanzibar – Nusu fainali

26- 9-1951
Tanganyika 1-0 Zanzibar – Nusu fainali

26- 9-1952
Zanzibar 3-1 Tanganyika – Kutafuta mshindi wa tatu

12-10-1955
Tanganyika 3-0 Zanzibar – Nusu fainali

30-11-1956
Zanzibar 3-2 Tanganyika – Kutafuta mshindi wa tatu

5- 9-1957
Zanzibar 3-3 Tanganyika – Kutafuta mshindi wa tatu(kwa kuwa walitoka sare, wakawana nafasi hiyo)

Kuanzia 1958 mpaka 1971, mashindano yalichezwa kwa mtindo wa mzunguko kama ligi. Mwenye pointi nyingi ndiyo alikuwa bingwa.

10-10-1958
Tanganyika 3-2 Zanzibar

3-10-1959
Tanganyika 2-2 Zanzibar

14-10-1960
Tanganyika 4-2 Zanzibar

6-10-1961
Tanganyika 3-0 Zanzibar

15-12-1962
Tanganyika 6-0 Zanzibar

4-10-1963
Tanganyika 2-1 Zanzibar

29- 9-1964
Tanganyika 3-1 Zanzibar- Tanzania bara wakawa mabingwa

NB: Huu ndiyo mwaka ambao Tanganyika na Zanzibar ziliungana miezi mitano kabla na kuzaa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jina la Tanzania lilianza kutumika Novemba Mosi 1964.

29- 9-1965
Tanzania 3-0 Zanzibar – Tanzania bara wakawa mabingwa

28- 9-1966
Zanzibar 0-4 Tanzania

10-10-1967
Zanzibar 3-0 Tanzania

5-10-68
Tanzania 3-0 Zanzibar

3-10-1969
Tanzania 3-0 Zanzibar

30- 9-1970
Zanzibar 1-2 Tanzania

2-10-1971
Tanzania 1-1 Zanzibar

Mwisho wa mfumo wa ligi.
Mwaka 1972 mashindano hayakufanyika, yakarudi 1973 kwa mtindo wa makundi.

25- 9-1973
Tanzania 1-0 Zanzibar – Kundi 2

1974 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti. Tanzania bara walikuwa mabingwa.

5-11-1975
Tanzania 4-0 Zanzibar – Kundi 2

1976 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

1977 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

1978 Tanzania Bara na Zanzibar hazikushiriki (mwaka wa vita vya Idd Amin)

16-11-1979
Tanzania 2-1 Zanzibar – Kutafuta mshindi wa tatu

1980 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

15-11-1981
Tanzania 3-1 Zanzibar

1982 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

1983 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

1984 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

1985 hazikukutana kwa sababu Zanzibar haikushiriki

1986 mashindano hayakufanyika

19-12-1987
Zanzibar 2-0 Tanzania – Kundi 1

12-11-1988
Zanzibar 1-0 Tanzania – Kundi 1

1989 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

8-12-1990
Zanzibar 0-0 Tanzania – Kundi 1

19-12-1990
Zanzibar 1-2 Tanzania – Kutafuta mshindi wa tatu

NB: Huu ndiyo mwaka pekee kukutana mara mbili

1991 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

Novemba 1992
Tanzania 0-1 Zanzibar

NB: Tanzania bara ilikuwa na timu 2, Victoria na Kakakuona. Iliyocheza na Zanzibar ilikuwa Victoria.

1993 mashindano hayakufanyika

1994 hazikukutana kwa sababu Zanzibar haikushiriki. Tanzania Bara walikuwa mabingwa.

1995 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti. Zanzibar walikuwa mabingwa.

1996 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

1997 mashindano hayakufanyika

1998 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

1999 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

2000. Zanzibar ilijitoa, Tanzania bara ilifungiwa na FIFA

2001 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

2002 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

2003 hazikukutana kwa sababu Tanzania bara ilijitoa

13-12-2004
Zanzibar 4-2 Tanzania

2-12-2005
Tanzania 1-1 Zanzibar

2006 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

2007 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

2008 mashindano yalichelewa kuanza, yakaanza Disemba 31 na kumalizika Januari 2009.
5- 1-2009
Tanzania 2-1 Zanzibar

1-12-2009
Tanzania 1–0 Zanzibar

2010 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti. Tanzania bara wakawa mabingwa.

2011 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti

8-12-2012
Tanzania 1-1 Zanzibar [5-6 pen]. Wachezaji wa Zanzibar wakagawana fedha za zawadi bila idhini ya viongozi wao.

2013 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti.

2014 mashindano hayakufanyika.

2015 hazikukutana kwa sababu zilikuwa makundi tofauti.

2014 mashindano hayakufanyika.

7-12-2017
Tanzania 1–2 Zanzibar

Kilimanjaro Stars yajiwinda dhidi ya Rwanda
Yondani kuikosa Rwanda, Mbaraka apata nafuu