Mwanamuziki Rich Mavoko anaendelea kutikisa kiberiti, akiunadi ujio wake mpya kwenye kiwanda cha muziki wa bongo fleva nchini baada ya ukimya kwa kipindi kirefu.

Baada ya ujumbe mfupi aliouchapisha kwenye mtandao wa Instagram siku ya jana machi 11, hatimaye leo machi 12 pia amerejea na ujumbe mwingine unaoonesha wazi kuwa amedhamiria kufanya kitu kikubwa na cha tofauti kwenye sanaa yake ifikapo Machi 18, 2022.

“Muda unakaribia, na huu mwaka ni wetu ✊?! Round hii ni muda wa kushinda mechi zote kwenye ligi kuu ya Bongo Flava. Kama Messi wa Bongo Flavani tunarudi uwanjani kuchukua makombe ?. Yote kuashiria mimi ni …………?”  Ameandika.

Mavoko ameweka ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kama sehemu ya kuwaarifu mashabiki wake kuhusu namna alivyojipanga kurejea kikamilifu.

Harmonize: Sijipendekezi kwa Bakhresa
Kamati yaundwa kuchunguzwa kuchafuka mto mara