Kiongozi wa Maybach Music Group, Rick Ross ameachiwa kutoka jela alipokuwa akishikiliwa kwa kosa la kuteka, kushambulia na kumtishia maisha.

Jaji wa mahakama ya Fayette ameamua kumuachia rapa huyo baada ya kukubali kulipa faini kwa kuweka bond (dhamana) yenye thamani ya dola milioni 2.

Kwa mujibu wa TMZ, dhamana hiyo inajumuisha dola milioni 1 ambayo ni thamani ya nyumba zake mbili, milioni 500 ya mdhamini na kiasi kingine cha dola milioni 500 fedha taslim.

Imeripotiwa kuwa rapa huyo aliweka ahadi ya kutofanya kosa lolote atakapokuwa uraiani na amefungwa mguuni kifaa maalum cha usalama cha kumonita mahali alipo (GPS ankle monitor).

Rick Ross alikamatwa na polisi Jumatano, Juni 24. Ripoti ya polisi ilieleza kuwa mlalamikaji aliwaeleza wana usalama kuwa alitishiwa kupigwa risasi na rapa huyo ambaye baadae alimteka na kumtesa.

Msikiti Wachangia Fedha Kukarabati Kanisa Lililoharibiwa Na Muislam
Ray C Anatafuta Mume Wa Kuishi Nae Milele, Ataja Sifa