Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete akerwa na tuhuma za watu wengi mitandaoni zinazosambaa kuhusiana na yeye kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya.
Hivi karibuni baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kumkabidhi mkuu wa kikosi cha kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga majina 97 ya watu wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo.
Mkuu wa mkoa huyo wakati wa kukabidhi majina hayo alidai wako vigogo wa biashara hiyo pamoja na watoto wa viongozi
Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Ridhiwani aliweka wazi namna ambavyo anaiunga mkono serikali katika vita ya dawa za kulevya.
Jumatano hii kupitia kurasa yake ya instagram ameamua kuandika na kuonesha jinsi anavyokerwa na tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya,”.
”Ni jambo jema na la faraja kubwa kwangu kama uchunguzi unafanywa. Ni ukombozi kwangu, Ukweli utajulikana kuwa ni uvumi tu usiokuwa na chembe ya ukweli,”
Ni maneno ya watu wasionitakia mem. Sina la kuficha. Sufanyi biashara hiyo haramu na wala sijawahi kufikiria kuifanya. Ni bora kufa maskini kuliko kutafuta utajiri kwa nji ahiyo,” ameandika mbunge wa jimbo la Chalimze, Ridhiwani Kikwete