Msanii wa muziki wa Pop nchini Marekani Rihanna Fenty ametoa ya moyoni kuhusu wachezaji wa soka ambao anawazimikia na kuwakubali kwa kile wananchokifanya katika soka.

Rihanna amesema kuwa kama ingekuwa kuolewa na mchezaji wa soka duniani basi angemchagua staa wa zamani wa klabu ya Manchester United na Real Madrid , maarufu kama David Beckham

Pia amesema kwa soka la sasa anamkubali sana Cristian Ronaldo na kumuweka pembeni Lionel Messi.

Msanii huyo amedai kuwa Beckham alimfanya apende soka na angekubali kuolewa na mchezaji huyo lakini aliwahiwa na Poah Spice  mke wa Bechkam, Victoria Beckham.

”Kwa sasa naweza kusema kuwa kwenye soka navutiwa na uwezo wa nyota Real Madrid, Christiano Ronaldo lakini miaka ya nyuma nilikuwa navutiwa na David Beckham, ningeweza kuolewa nae kama angekuwa tayari lakini nimewahiwa na victoria Beckham” amesema Rihanna.

Msanii huyo ameongeza kuwa hakuwa na ndoto za kuja kuwa msanii bali siku zote katika maisha yake amekuwa akiwa ndoto za kuja kufanya kazi benki , kuwa mwalimu , mwanamitindo, mambo ya anga na kuigiza

Ben Pol ataja chanzo cha kumzimia simu Ebitoke
Dortmund kuivaa Real Madrid leo