Mwanamuziki  Rihanna pamoja na mpenzi wake rapa ASAP Rocky wameweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto siku za usoni.

Wawili hao wameonekana kupitia picha zilizoenea kote mitandaoni zikiwaonyesha wakiwa huko Harlem mji aliozaliwa rapa ASAP Rocky, nchini Marekani.

Rihanna na Rocky

Rihanna akiwa amevalia mavazi ambayo yameruhusu sehemu ya tumbo lake kuwa wazi kiasi cha kudhihirisha kuwa nyota huyo ni mwenye ujauzito.

Rihanna na ASAP Rocky wamewahi kuwa marafiki kwa miaka kadhaa, kabla ya kuanza mahusiano yao rasmi mwishoni mwa mwaka 2020, ambapo tangu hapo wameonekana kuwa pamoja wakati wote.

Ahmed Ally: Sikupata tabu kujiunga Simba SC
Mbeya City yatuma salamu Young Africans