Moja ya habari kubwa kutokea nchini Marekani ni kuenea kwa kasi tetesi za mwanamuziki Rihanna kuachana na mpenzi wake Asap Rock ambaye ndio baba mtoto wake mtarajiwa.
Taarifa zinasema kuachana kwao ni baada ya Riri kuwa amemfumania Asap akimsaliti na mmoja wa wabunifu wa viatu kutoka katika kampuni ya Fenty aitwaye Amina Mauddi.
Taarifa hizo zimeenea kwa kasi kote mitandaoni hasa katika mtandao wa twitter baada ya mtumiaji mmoja wa mtandao huo kuvujisha taarifa hiyo jambo lililofanya idadi kubwa ya mashabiki na wafuatiliaji wa wapenzi hao kuanza kutiririsha maoni kuhusu kinachoendelea.
Katika maoni hayo baadhi ya vyanzo vimedhihirisha kuwa pengine kukawa na kuna ukweli kuwa wawili hao hawako pamoja tena kufuatia tukio hilo.
Asap Rock na Rihanna siku za hivi karibuni wamekuwa wakiingia kwenye mijadala kama wapenzi wanaovutia tangu wawili hao kuweka bayana kuwa wanatarajia kupata mtoto siku za usoni.