Miezi minne baada ya kuachana na nyota wa muziki wa bongo fleva, Diamond Platinum na mpenzi wake, Zari Hassan, msanii wa muziki wa Injili nchini Kenya, Alex Apoko ,maarufu Ringtone ameonyesha nia ya kumchumbia mama huyo wa watoto watano.
Ringtone anayetamba na wimbo wake wa ‘Tenda Wema’ aliyeimba na msanii kutoka Tanzania Christine Shusho amesema kuwa yeye ndio suluhu kwa matatizo ya kimapenzi ambayo yamekuwa yakimzonga mfanyibiashara huyo wa Uganda.
Msanii huyo sasa amemtaka mfanyabiashara huyo kutokubali kumrudia Diamond Platinum na badala yake kukubali uchumba wake kwa lengo la kumtumikia Mungu.
”Diamond aniachie Zari, Zari ni wangu wa Moyoni, atuache tumtumikie Mungu kwakuwa yeye kashindwa kumtunza Zari, kwa sasa huyu ni wangu,” amesema Ringtone
Hata hivyo, Zari na Diamond waliachana siku ya wapendanao ya Valentine mwaka huu baada ya kudai kwamba nyota huyo wa muziki wa bongo amekuwa akimdhalilisha kupitia uhusiano na wanawake wengine.