Aliyewahi kuwa beki na nahodha wa kikosi cha Man Utd Rio Ferdinand, amempa somo kiungo wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC Paul Pogba, ambaye anapigiwa upatu wa kutua Old Trafford katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Pogba amekua gumzo kwa majuma kadhaa, kufuatia usajili wake wa kurejea Old Trafford ambao utaigharimu Man Utd kiasi cha Pauni milion 100.

Ferdinand alihojiwa na gazeti la Daily Star, na kutoa maoni yake kuhusu usajili wa kiungo huyo ambaye aliwahi kupita Man Utd kabla ya kuruhusiwa kuondoka mwaka 2012.

“Wakati Pogba amedhamiria kuondoka Old Trafford nilibahatika kuzungumza nae na nilimuuliza kwa nini alidhamiria kufanya hivyo, jibu alilonipa alikua anahitaji kuwa mchezaji bora dunaini.’Naamini dhamira yake imetimia na jambo hilo haliwezi kupingwa na mtu yoyote.

“Je thamani yake ni kiasi cha Pauni milioni 100? Nafikiri inawezekana lakini sio kwa uzito mkubwa, kinachofanywa hapa ni kama miujiza ambayo imetengenezwa kwa makusudi na viongozi wa klabu ya Juventus ambao walijitahidi kuipandisha thamani ya Pogba.

Hata hivyo Ferdinand amemshauri Pogba kuwa makini na kiwango chake cha soka kwa kuhakikisha anaisaidia klabu ya Man Utd kwa kucheza vyema na kujituma wakati wote ili kufanikisha harakati za kurejesha heshima klabuni hapo.

Alisema ni vigumu kwa kila shabiki wa soka wa Man Utd pamoja na wengine duniani kuamini thamani ya Pogba, lakini kwa mchezaji husika hana budi kuwaminisha kwa kuonyesha ikiwnago chake anapokua uwanjani.

“Pogba hatokua na nafasi nyingine wa kudhihirisha thamani yake zaidi ya kucheza vyema uwanjani na kuwaridhisha waliokua na wasiwasi na kiasi cha pesa ambacho kinaendelea kutajwa kwa sasa kama ada yake ya usajiali”

Usajili wa Paul Pogba kuerejea Man utd bado ni kitendawili kutokana na taarifa zinzoendelea kuibuka kila kukicha, kufuatia mazungumzo baina ya viongozi wa mashetani wekundu, Juventus pamoja na wakala wake mchezaji huyo (Mino Raiola) kutokua sawa sawa.

Rafa Benitez Akubali Yaishe, Amfungulia Milango Moussa Sissoko
Everton Wabadili Gia Angani, Wapanga Kumbakisha Lukalu