Mnyanyua vitu vizito kutoka nchini Armenian Andranik Karapetyan, jana jioni alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kupata maumivu makali ya mkono wake wa kushoto kufuatia kuzidiwa na chuma cha uzito wa kilo 195.

Karapetyan mwenye umri wa miaka 20, alianza kubeba kwa usalama chuma hicho na kilipokifikisha usawa wa kichwa cheke alionekana kuzidiwa uzito na alipojaribu kukitua kilimshinda na kuelelemea sehemu ya mgogoni.

Tukio hilo lilimsababishia mkono wake wa kushoto kugeuka mara mbili katika sehemu za kiviko.

Maafisa waliokua wanasimamia mchezo wa kunyanyua vitu vizito alijaribu kumpatia huduma ya kwanza kabla ya kumkimbia hospitalia.

Andranik KarapetyanAndranik Karapetyan akiachia chuma kwa nyuma.

Andranik KarapetyanAndranik KarapetyanAndranik KarapetyanAndranik Karapetyan akiwa anaugulia maumivu ya mkono wake wa kushoto.

Karapetyan alikua akishindana na mshiriki kutoka nchini Kazakhstan Nijat Rahimov aliyeshinda medali ya dhahabu, Lyu Xiaojun (China) mshindi wa medali ya fedha na Mohamed Mahmoud (Misri) mshindi wa medali ya shaba.

Tukio la kushindwa na uzito, pia lilimtokea mshiriki wa kike kutoka nchini China, Xiang Yianmei aliyekua amebeba chuma cha kilo 118, lakini kwa bahati nzuri hakupata maumivu makali kama ilivyo kuwa kwa Karapetyan.

Jack Wilshere: Mashabiki Watakua Na Haki Ya Kutuzomea
Pamoja Na Kuwasili Kimya Kimya, TFF Yawashtukia Mo Bejaia