Siku 10 kabla ya kumalizika kwa michezo ya Olimpiki ambayo inafanyika nchini Brazil na kuhusisha wanamichezo zaidi ya 11,000, wanamichezo mbalimbali wameendelea kufanya vizuri na kushinda medali na wengine wakitengeneza historia mpya katika michezo hiyo.

Kyle Chalmers ameweka rekodi ya kuwa mwogeleaji mdogo kushinda medali ya dhahabu na pia kuvunja rekodi iliyokuwepo kwa miaka 48 ya kuwa raia wa Australia kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya kuogelea kwa mita 100, jambo ambalo mara ya mwisho lilifanywa na Michael Wenden, 1968 wakati mashindano hayo yalipofanyika Mexico.

Chalmers alimaliza mita 100 katika kuogelea kwa kutumia sekunde 47.58 akifuatiwa na Mbelgiji, Pieter Timmers aliyetumia sekunde 47.80 na kupata medali ya fedha na Nathan Adrian akishika nafasi ya tatu baada ya kumaliza kwa kutumia sekunde 47.85 na kupata medali ya shaba.

Akizungumzia ushindi huo, Chalmers alisema, “Kiukweli sikuwa najua kama ninaweza kushinda, mimi sio mtu ambaye najihusisha sana na kuogelea, nimekuwa nikifanya mambo mengine kabisa kama kucheza basketball na soka”

“Nafahamu tumekuwa tukikosa ushindi na hilo lilinifanya kuongeza spidi, nilitaka kushinda kwa ajili yangu na familia yangu na nchi yangu na kwa marafiki zangu wote wa nyumbani”

Young Africans Wasubiri Maamuzi Ya FIFA
Waarabu Kuamua Game Ya Super Eagles Vs Taifa Stars