Mamlaka Huru ya Kusimamia Shughuli za Kipolisi nchini Kenya (IPOA), imesema kuwa watu 15 waliuawa na polisi na wengine 31 walijeruhiwa tangu nchi hiyo ilipoanza hatua ya kuzuia watu kutoka majumbani kuanzia jioni (curfew) ili kupambana na mlipuko wa virusi vipya vya corona (covid-19).
Ripoti ya IPOA iliyotolewa jana, imeeleza kuwa kulikuwa na malalamiko 87 ambayo yamehusisha mauaji, ufyatuaji wa risasi, vipigo, wizi na unyanyasaji wa kingono ambayo yanaendelea kufanyiwa uchunguzi.
“Baada ya uchunguzi wa awali, imebainika kuwa watu 15 waliuawa, 31 walijeruhiwa na kwamba yote hayo yalihusishwa moja kwa moja na vitendo vya maafisa wa polisi wakati wa kutekeleza amri ya watu kutotoka majumbani majira ya usiku (curfew),” Mwenyekiti wa IPOA, Anne Makori amekaririwa na Citizen TV.
IPOA pia imesema wameanza kufuatilia kwa ukaribu hali zilizopelekea watu kujeruhiwa katika matukio mengine sita.
Matukio hayo ni pamoja na matukio mawili katika Kijiji cha Katanini, Kaunti ndogo ya Kabiyet yaliyotokea Mei 29 2020. Tukio lingine ni la mtu mmoja kupigwa risasi katika eneo la Mathare, Nairobi, Juni 1, 2020, na watu watatu wa familia moja kupigwa risasai katika eneo la Kwale, Mei 30, 2020. Pia, tukio la mwanamke mmoja kushambuliwa kwa risasi katika eneo la kizuizi cha polisi huko Emali, Mei 31, 2020.
“Tutakapokamilisha uchunguzi wetu, na kwa mujibu wa Kifungu cha 6(a) cha Sheria, Mamlaka hii itatoa mapendekezo ambayo yatajumuisha kufungua mashtaka dhidi ya watuhumiwa kwa upande wa maafisa wa polisi,” imeeleza taarifa ya IPOA iliyosaniwa na Mwenyekiti huyo.
Ujumbe wa B12 kabla ya kuikacha Clouds FM kuhamia E-FM
Bei ya mafuta yaporomoka, orodha kamili ya bei kwa kila mkoa iko hapa