Pengo kati ya matajiri na masikini duniani imeendelea kujidhihirisha ambapo takwimu zilizotolewa hivi karibuni na shirika la OxFam unaonesha kuwa asilimia moja tu ya matajiri wanamiliki utajiri unaozidi mali za watu wengine wote duniani zikijumlishwa.

Ripoti hiyo ya OxFam imebaini pia kuwa matajiri 62 pekee wanamiliki utajiri ambao ni mkubwa sawa na jumla ya mali za asilimia 50 ya watu wote masikini duniani.

Oxfom iliweka kipimo cha utajiri wa dola za kimarekani 760,000 kuwa kipimo cha utajiri wa kundi la watu waliowekwa katika kundi la kwanza lililozaa asilimia 1 iliyotajwa.

Graph

Shirika hilo limetumia takwimu hizo kuwashauri viongozi wa dunia waliokutana mjini Davos nchini Uswizi kuchukua hatua zitakazosaidia kupungua pengo hili kubwa la kiuchumi kati ya watu matajiri na masikini duniani.

Kadhalika, shirika hilo limeshauri kupunguza pengo la tofauti kati ya ulipaji wa mishahara kwa misingi ya jinsia, pamoja na kuweka usawa katika uridhi wa mali kati ya wanawake na wanaume.

Chanzo: BBC

 

 

Picha: Waliokumbwa na Bomobomoa Mkwajuni wafunga barabara na kufanya fujo
Azam FC Waifuata JKT Mgambo Tanga