Ripoti zilizotolewa hivi karibuni zimeonesha kuwa bilionea muuza madawa ya kulevya wa Mexico, Joaquin Guzman maarufu kama ‘El Chapo’ alifanya mapenzi mara 46 akiwa gerezani humo kabla ya kutoroka.

Ripoti hiyo ilionesha kuwa tajiri huyo alitembelewa na wanawake kwa ajili ya kufanya naye mapenzi ‘Conjugal Visit’ mara 46 kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu aliokaa katika gereza lenye ulinzi mkali nchini humo kabla ya kutoroka Julai mwaka huu.

Ripoti hiyo imechapishwa kwenye jarida la Mexico la Proceso baada ya mwandishi wa jarida hilo, Alejandro kufanya mahojiano na maafisa husika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Mexico walifahamu mpango wa El Chapo kutoroka katika gereza hilo lakini hawakuchukua hatua.

El Chapo alifanikiwa kutoroka kwenye gereza hilo Julai mwaka huu kupitia kwenye bomba linalotoa maji machafu kutoka gerezani humo kwenda baharini.

Watu 14 Wauwawa Kwa Risasi Marekani
Uongozi wa Chadema wazungumzia Kasi ya Magufuli