Ripoti ya wataalamu waliokodiwa na familia ya George Floyd aliyeuawa na polisi nchini Marekani, imetofautiana na ripoti ya Serikali, ingawa zote zimehitimisha kuwa aliuawa na polisi.

Kampuni ya uchunguzi ya kujitegemea iliyokodiwa na familia yake imeeleza kuwa Floyd alifariki baada ya damu yake kushindwa kuzunguka akiwa amekandamizwa shingoni na afisa polisi wa Minneapolis, wiki iliyopita. Imeeleza kuwa mkandamizo huo ulikata mzunguko wa damu kwenda kwenye ubongo.

Lakini, Ripoti ya wataalamu wa Serikali kutoka Kaunti ya Hennepin iliyotolewa jana, ilieleza kuwa Floyd alifariki baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi pamoja na mkandamizo kwenye shingo.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa Floyd alikuwa na matatizo ya moyo ambayo yalichangia kupoteza maisha kwenye tukio hilo, jambo ambalo Ripoti ya watalaamu wa kujitegemea halikubainishwa. Pia, wataalam wa Kaunti ya Hennepin hawakueleza kuhusu Floyd kupoteza uwezo wa kupumua kutokana na mkandamizo.

Mwanasheria wa Familia ya Floyd, Antonio Romanucci ameiambia CNN kuwa utofauti wa ripoti hiyo hauondoi uhalisia wa kosa kuwa ameuawa na polisi.

“Iwe aimesababishwa na hali gani aliyokuwa nayo au la, hiyo haina maana kwa kifo cha chake ambacho kimetokana na kipigo, ambacho ni kifo kilichosababishwa na mtu mwingine,” alisema. “Matokeo ya mwisho ambayo ni kwamba George Floyd amefariki, hayatakuwa na utofauti wowote,” aliongeza.

Floyd mwenye umri wa miaka 46, alifariki baada ya kukandamizwa shingoni kwa goti na askari polisi. Kwakuwa Floyd ni mtu mweusi na ameuawa na askari mweupe, imeubua hisia za ubaguzi wa rangi katika mauaji hayo.

Tukio hilo limeibua maandamano nchini Marekani. Waandamanaji wamepambana na askari katika maeneo mengi wakitaka hatua kali ichukuliwe kwa mhusika na kupinga unyanyasaji wowote. Maandamano hayo yamepewa kauli mbiu ya ‘I can’t Breathe’, neno alilokuwa analitumia Floyd alipokuwa amekandamizwa na polisi.

Simba SC waingia hatua mpya
Popat: Tuna kiu ya ubingwa