Zaidi ya wanafunzi 20 walifoanya mitihani ya kuhitimu elimu ya Sekondari mwaka huu katika Kaunti ya Bomet nchini Kenya wamebainika kuwa walikuwa wajawazito.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Kaunti hiyo, kati ya wanafunzi hao wa kike, 13 walikuwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Monica.
Kamishna wa Kaunti ya Bomet, Geoffrey Omondi ameeleza kuwa wamebaini baadhi ya wanafunzi wajawazito walifanya mitihani hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Longisa.
“Ripoti hii inaogofya na tutatumia maafisa wa CID kufanya uchunguzi zaidi na kutoa taarifa za kina na watu waliohusika watakamatwa,” alisema Kamishna.
Aidha, Kamishna alifafanua kuwa idadi kubwa zaidi ya wasichana waliokuwa na ujauzito katika mitihani hiyo ni wale wanaotoka katika Shule za wasichana pekee kwa kulinganisha na wale wanaotoka shule za mchanganyiko.