Umoja wa Kitaifa wa Kutoa Ushauri wa Kitaaluma nchini Kenya (NACADA), umetahadharisha kuwa tabia za watu kunywa pombe wakiwa majumbani kwao ni hatari, baada ya Serikali kuzuia watu kukaa katika sehemu za starehe.

Kupitia ripoti yao ya mwenendo wa hatua za kukabiliana na covid-19 nchini humo na madhara yake, NACADA imeeleza kuwa watoto wengi wanaweza kujenga tabia za kuwa walevi, kutokana na kuwaona wazazi wao wakinywa pombe.

“Kunywa pombe majumbani pia ni hatari kwa mazingira ya familia hasa kwa watoto na wanafunzi ambao pia wako nyumbani kwa sababu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya corona,” Mwenyekiti wa NACADA, Profesa Mabel Imbuga.

“Tunawashauri wazazi kuchukulia hatua hii kwa mtazamo chanya, kwa kutumia muda huo na katazo hilo kuachana na pombe na kujiweka karibu zaidi na watoto,” aliongeza.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Wizara ya Afya kueleza mpango wa kuongeza hatua kali zaidi kuhusu uuzwaji na unywaji wa pombe. Wizara imepiga marufuku watu kukaa kwenye maeneo ya starehe na kunywa vinywaji, badala yake wanunue na kwenda navyo nyumbani.

Video: Mwili wa Mkapa kutoka Lugalo – Uwanjani

Familia yasema ugonjwa uliomwondoa Mkapa

Mtuhumiwa mauaji ya kimbari Rwanda aonekana mtaani, vyombo vya habari 'vyamchoma'
Picha: Viongozi wakiaga mwili wa Mkapa uwanja wa uhuru