Ripoti ya utafiti wa Viwango vya Furaha Duniani 2016 ambayo hutolewa kila mwaka na shirika la maendeleo endelevu (Sustainable Development Solutions Network (SDSN)) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa, imebaini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kwenye orodha ya nchi zenye furaha.

Utafiti huo ulitumia vigezo vya pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi, kuwa huru dhidi ya ufisadi, na ukarimu miongoni mwa jamii.

Kitu kilichowashangaza wengi ni Tanzania kuzidiwa na nchi mbalimbali ambazo ziko katika vita na machafuko ama zikikabiliwa na baa la njaa ikiwemo Somali ambayo imeshika nafasi ya 76 huku Tanzania ikishika nafasi ya 149 kati ya nchi 157.

Nchi za Mwisho kwa furaha duniani

Mbali na Tanzania, nchi nyingine Kumi zilizoko kwenye orodha hiyo ni Madagascar, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria, na Burundi ambayo imekuwa ya mwisho.

Ripoti hiyo iliyotolewa Mjini Roma nchini Italia siku tatu kabla ya Dunia kuadhimisha siku ya furaha duniani (Machi 20), imeitaja Denmark kuwa nchi inayoongoza kwa wananchi wake kuwa na furaha zaidi duniani.

Zipo baadhi ya nchi ambazo tayari zimeteua mawaziri wa ‘Furaha’ ikiwemo Venezuela. Waziri wa Furaha hushughulika kuhakiksha wananchi wanaongeza furaha kila siku.

Hizi ni nchi 10 zenye furaha zaidi duniani:

1. Denmark
2. Switzerland
3. Iceland
4. Norway
5. Finland
6. Canada
7. Netherlands
8. New Zealand
9. Australia
10. Sweden

Magufuli amtumia Muhongo kuiondoa IPTL iliyozaa sakata la Escrow
Balozi Mwapachu: Nililewa Mahaba ya Lowassa na ahadi yake kwangu, nilikosea