Ripoti mpya iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani Duniani, (SIPRI) yenye makao yake makuu Stockholm Sweden imebainisha kuwa ununuzi wa silaha umeongezeka duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, imesema kuwa biashara ya silaha duniani na huduma za kijeshi vimeongezeka kwa mwaka 2016 ikiwa ni mara ya kwaza katika kipindi cha miaka mitano.

Aidha, imesema kuwa wanufaika wakubwa katika biashara hiyo ni makampuni makubwa yanayojihusisha na utengenezaji silaha kutoka Marekani na Ulaya.

Hata hivyo, ripoti hiyo imeongeza kuwa, Kampuni kubwa ya utengenezaji wa silaha duniani, LOCKHEED MARTIN, ilipata faida kubwa kwa kuziuzia silaha mpya ya F- 35, huku mteja wake mkuu ni jeshi la Marekani.

 

 

 

Mwambusi ailaumu TFF kushindwa kwa Timu ya Taifa
LIVE DODOMA: Rais Dkt. Magufuli katika Mkutano wa 9 wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania