Ripoti ya kamati ya bunge nchini Uingereza imekosoa hatua ya Uingereza na Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya mwaka 2011.

Kamati hiyo ya Mambo ya Nje imesema Uingereza iliongeza chumvi ilipokuwa inaeleza hatari ambazo zinge wakumba raia baada ya serikali ya Gaddafi kuanza kukabiliana na waasi.

Msemaji wa serikali ya Uingereza ametetea serikali na kusema muungano wa mataifa ya Kiarabu, Arab League, pamoja na Umoja wa Mataifa, wote waliunga mkono hatua hiyo ya kijeshi.

Ripoti hiyo pia Inamtuhumu aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kwa kukosa kuandaa mpango mkakati  wa kuisaidia Libya.

Wabunge hao wamesema hilo lilisababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, mzozo wa wahamiaji, ukiukwaji wa haki za binadamu na kukua kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wanaojiita Islamic State Afrika kaskazini.

FA Yamuweka Kikaangoni Mark Hughes
Wabunge wakatwa Posho ya Siku ‘kuwashika mkono’ wahanga wa tetemeko la Ardhi