Ripoti imeitaja India kuwa nchi hatari zaidi duniani kwa wanawake kwasababu ya kuwa na kiwango kikubwa cha ukatili dhidi ya wanawake na ubakaji.
Ripoti ya Thomson Reuters Foundation iliyochapishwa jana, iliyofanya mahojiano pia na watalaam 550 kwenye masuala ya wanawake pamoja na unyanyasaji majumbani, utumwa wa kingono na ndoa za kulazimishwa, imeonesha kiwango kikubwa zaidi cha matukio ya kikatili dhidi ya wanawake kinaripotiwa nchini India.
India imetajwa kwa mara nyingine baada ya mwaka 2012 kutajwa kuwa katika nafasi ya nne kati ya nchi saba zilizochaguliwa kufanyiwa utafiti zikiwa na kiwango kikubwa cha ukatili dhidi ya wanawake. Matukio yaliyotajwa wakati huo pamoja na vigezo vya mwaka huu ni ndoa za utotoni, vipigo na ukeketaji.
Dunia iliwahi kushtushwa na tukio la ajabu la ubakaji mwaka 2012 baada ya kundi la wanaume kumbaka kwa kupokezana kwenye basi mwanafunzi wa kike jijini New Delhi.
- Afungwa jela kwa kuuza nyama ya paka kwa miaka saba
- Wizara ya Afya yatoa tahadhari ugonjwa wa Dengue, Chikungunya
Ingawa matukio hayo yaliamsha hasira ya dunia na kulaani vitendo vya ubakaji, Shirika la kudhibiti jinai nchini humo limeeleza kuwa wastani wa kesi 100 za unyanyasaji wa kingono huripotiwa kila siku.