Kufa kufaana, ndivyo tunavyoweza kusema baada ya Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu kudai Dereva wake ambaye alikuwa naye siku ya tukio wakati akipigwa risasi Septemba 17, 2027, Adam Bakari kupata kazi na kuishi nchini Ubelgiji.
Lissu, ambaye alikuwa akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media amesema, mara baada ya kutokea kwa tukio hilo Adam hakujua afanye nini na Polisi walipoanza kumtafuta kwa nia ya kumhoji aliogopa kutokana na vyanzo mbalimbali kudai kuwa naye angepotea hivyo kuamua kusafiri hadi Nairobi nchini Kenya kuepuka majanga.
“Dereva wangu alikuwa hajawahi kutoka Tanzania, kabla ya mimi kushambuliwa hakuwa na paspoti wala chochote na yalipoanza kutoka toka maneno tukimpata Dereva wake hadithi ya Mbowe itakamilika, Dereva apatikane afanywe aongee na atarekodiwa video aseme ni Mbowe kwahiyo ikambidi aje Nairobi akakaa nami,” anasimulia Lissu.
Aidha amebainisha kuwa, “sasa ikafikia kipindi mimi natakiwa kupelekwa Ulaya kwa matibabu tukauarifu ubalozi wa Ubelgiji na akapatiwa viza ya kibinadamuda kwenda pahala pengine na utaratibu wake wa maisha ya Ubelgiji yalikuwa tofauti na ya kwangu wakamtunza kumfundisha lugha na kumpatia kazi yaani kitu kibaya kilichonitokea kimezaa matunda mema kwake.”
Alipoulizwa na mwandishi kuhusu kukimbia mapambano kwa kwenda nje ya nchi na kama wana uwezo wa kuiomboa nchi kama anavyodai, Lissu alisema “anayepigana na kukimbia anaishi, ili aweze kupigana tena kesho,” maneno ambayo ameyanukuu toka kwenye wimbo wa marehemu Bob Malrey wa “‘He who fights and run away, live to fight another day.”