Msanii wa filamu na vichekesho nchini , Riyama Ally amefunguka jinsi alivyofurahi kupewa heshima na wasanii Roma Mkatoliki na Stamina wanaounda kundi la Rostam kwa kuingiza kionjo katika wimbo wao ‘kaolewa’ kionjo ambacho kimefanya wimbo kunoga zaidi.

Mwanadada huyo amesema kwake ni heshima kubwa lakini pia amefurahi kuona wimbo umepokelewa vizuri hata kama sio wa kwake lakini ameweka mkono wake pale na wimbo  umekuwa ukifanya vizuria ambapo hadi kufikia sasa nyimbo hiyo imeangaliwa na watu Milioni 1 na kuingia 10 bora nyimbo zinazoangaliwa zaidi katika mtandao wa Youtube.

”kabla ya wimbo kutoka meneja wa Rostam alinipigia simu akaniambia kuwa kuna sauti inatakiwa kuigizwa kwenye wimbo na mimi ndio mhusika, nikafika studio nikaingiza kile kionjo chini ya usimamizi wa mume wangu nashukuru sana kwa sababu wimbo umetoka na umependwa”

Mwanadada huyo anaeonekna kuwa na Vipaji vingi amekuwa moja ya chachu za sanaa kwa kazi zake nzuri anazofanya zinazoendana na uhalisia.

Serikali kuimarisha matumizi ya Fukwe
Eden Hazard: Luca Modric anastahili Ballon d'Or 2018