Aliyekua kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa pamoja na klabu ya Arsenal, Robert Emmanuel Pirès, ameingai katika harakati za kumshawishi mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England, Leicester City,  Jamie Vardy ili aharakishe kufanya maamuzi ya kujiunga na The Gunners.

Pires ambaye aliitumikia Arsenal kuanzia mwaka 2000–2006, amesema anaamini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miama 29 ana viwango vyote vya kuitumikia klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London.

Pires ambaye ni sehemu ya wachezaji waliokuwa vipenzi wa Arsene Wenger, wakati akiwa Highbury anaamini Vardy atafanya vizuri atakapokamilisha mpango wa kujiunga na Arsenal, hivyo anapaswa kufanya maamuzi ya haraka.

“Hakuna sababu kwanini ashindwe kufanya kazi,” alisema mshindi huyo mara mbili wa taji la Ligi Kuu ya England.

“Amefunga mabao mengi kwenye Ligi Kuu msimu uliopita na sasa anajulikana dunia nzima.” Alisema Pires

Vardy anatarajiwa kufanya maamuzi baada ya fainali za Euro 2016 zinazoendelea nchini Ufaransa, kufuatia klabu ya Arsenal kudaiwa kumtengea Pauni milioni 20.

Vardy alifunga mabao 24 kwenye Ligi ya England msimu wa 2015/16 na kuchangia kwa akiasi kikubwa hatua ya klabu ya Leicester City kutwaa ubingwa wa kwa mara ya kwanza.

Neymar da Silva Santos Júnior Akubali Yaishe
Simba SC Kumuajiri Kocha Aliyetwaa Kombe La Dunia