Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewajibu baadhi ya wadau wengi wa Soka la Bongo wanaona kuwa safari yao imefikia mwisho katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kwa kusema kikosi chake kina uwezo wa kufanya maajabu ugenini.

Simba SC itacheza mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali ugenini Casablanca-Morocco Jumamosi (April 29), ikiwa na mtaji wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa juzi Jumamosi (April 22) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amesema licha ya ubora wa Wydad AC lakini haimaanishi kuwa wao tayari wameshatoka katika mbio za kwenda Nusu Fainali kwani wanao uwezo wa kupaa matokeo na kisha wakawashangaza watu ambao wanaona kuwa tayari wameshatolewa baada ya ushindi wa bao 1-0.

“Watu wanaona kama safari yetu imeishia hapa mara baada ya kushinda bao 1-0, nataka niwaambie kuwa kwenye mpira kila kitu kinawezekana hivyo Simba tunaweza kuwashangaza watu nchini Morocco nkwa kupata matokeo mazuri.”

“Tutakwenda kwa nguvu zote na kupambana kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri na kufuzu nusu fainali, tunafahamu kuwa tunakwenda kukutana na timu ambayo ni bora na tunawaheshimu kwa kuwa ni mabingwa watetezi hivyo tutaend tukiwa na tahadhari kubwa sana,” amesema kocha huyo.

Robertinho anakumbukwa kwa kuwaondoa TP Mazembe kwao nchini DR Congo akiwa kocha mkuu wa Vipers SC, jambo ambalo anaamini kuwa wataweza pia kuwaondoa Wydad AC wakiwa kwao Morocco.

Utawala bora pekee hautoshi kuwahudumia wananchi - Othman
Aliyempa mwenzake Milioni 118 ajinyonga, aacha ujumbe