Kocha Mkuu wa Simba SC, Oliveira Roberto ‘Robertinho’ amekiri kikosi kina changamoto eneo la ulinzi, na kipindi hiki cha mapumziko ameanza kuifanyia kazi ili timu ikirudi uwanjani iwe imefunga busta zinazoenda sawa na eneo la viungo na ushambuliaji.

Simba SC imecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara ikifunga mabao sita na kuruhusu mawili katika ushindi wa mabao 4-2 mbele ya Mtibwa Sugar kabla ya kuifumua Dodoma Jiji 2-0, na kocha huyo amesema anapambana kupata kikosi cha kwanza, lakini maeneo mengine yapo freshi isipokuwa ulinzi.

Timu inafanya vizuri eneo la ushambuliaji wachezaji wanafunga, ila ukuta unashindwa kulinda na hili nalifanyia kazi tukirudi kwenye mashindano tuwe bora zaidi kuendeleza rekodi ya kuruhusu mabao machache kama msimu uliopita,” amesema.

“Huwezi kuwa na dosari eneo moja, wakati ukiwa bora jingine ni lazima kuwe na mizani sawa. Itafika wakati wachezaji watashindwa kuelewana kutokana na makosa yanayofanyika kuruhusu idadi kubwa ya mabao ya kufungwa, licha ya kufunga mengi.”

Robertinho amesema anahitaji safu bora ya ulinzi ili kuendana na kasi na ubora wa ligi msimu huu kutokana na namna alivyoona timu zilivyofanya usajili mzuri.

Pochettino akataa katakata ishu la Lukaku
Beckham afunguka upangaji matokeo