Baada ya kuambulia kisago cha mabao 5-1 juzi Jumapili (Novemba 05), Uongozi wa Klabu ya Simba SC umetangaza kusitisha mkataba wa Kocha Mkuu Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Taarifa iliyochapishwa katika vyanzo vya habari vya Simba SC zinaeleza kuwa, maamuzi hayo, yamefikiwa kwa makubaliano ya pande zote mbili, huku yakimuhusisha Kocha wa Viungo Corneille Hategekimana.

Hata hivyo maelezo hayo hayakufafanua sababu sahihi ya kuondolewa kwa kocha huyo kutoka nchini Brazil, licha ya kutajwa kichapo kilichotolewa na Young Africans kuendelea kuwa gumzo.

Taarifa ya Simba SC inaeleza: Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Pep Guardiola awajaza hasira wachezaji wake
Wakandarasi wazawa wanashiriki Ujenzi Bomba la Hoima - Kapinga