Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema baada ya sare ya mabao 2-2 dlhidi ya Power Dynamos mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa hajafurahishwa na safu yake ya ushambuliaji anarudi kwenye uwanja wa mazoezi kutibu tatizo hilo.

Kocha Roberto COliveira alisema safu yake ya ushambuliaji haikufanya vizuri sana, lakini anaenda kuyafanyia kazi maeneo mawili umakini kwenye safu ya ulinzi pamoja eneo la ushambuliaji ambalo limeshindwa kumpa kile alichokitaka.

“Nawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya katika mchezo huu licha ya kupata sare, tumecheza vizuri hasa kipindi ha pili, tumetengeneza nafasi nyingi. Tumepoteza nafasi zaidi ya tano za kufunga lakini huu ndio mpira wa miguu tunarudi nyumbani kujipanga,” alisema Robertinho.

Alisema kipindi cha kwanza hawakucheza vizuri na kuwapa nafasi Power Dynamos kumiliki mpira na kipindi cha pili alifanya mabadiliko ambayo yalimsaidia kucheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi hawakuzitumia.

Aliongeza kuwa sare waliyoipata ugenini ni matokeo mazuri na wanarudi katika uwanja wa mazoezi kufanyia kazi mapungufu yao ikiwemo safu ya ulinzi kulingana na mabao waliyofungwa na ushambuliaji kuwa makini na nafasi wanazotengeneza kutumia ipasavyo katika mechi ya marudiano ili kufuzu kucheza makundi.

Kocha wa Power Dynamos, Mwenya Chipepo alisema kuwa ulikuwa mchezo mzuri kila timu ilitengeneza nafasi na kuzitumia lakini kwa upande wao sio matokeo waliyoyatarajia wanarudi kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marejeano.

“Malengo yetu yalikuwa kupata ushindi nyumbani tukatafute sare ugenini lakini imeshindikana hivyo tuna kazi ya kufanya ili kuhakikisha tunapata ushindi na kusonga mbele.

Tulikuwa na nafasi ya kushinda nyumbani lakini kosa dogo lililofanywa na walinzi wangu dakika za mwisho imeufanya mchezo wa marejeano kuwa mgumu tutakapokuwa ugenini,” alisema Chipepo.

Katika mchezo huo wa Juzi Jumamosi (Septemba 16), Mabao ya Simba SC kwenye mhezo huo yalifungwa na Clatous Chama dakika ya 59 na dakika ya nyongeza ya 93 wakati Power Dynamos walifunga dakika ya 20 kupitia kipa Joshua Mutale na Cephas Mulombwa dakika ya 75.

Joao Félix: Ninafurahia maisha FC Barcelona
Martin Odegaard kukusanya mabilioni Arsenal