Baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema bado anaendelea kupambana ili kupata kikosi cha kwanza.

Simba SC imeshacheza michezo miwili ya Ligi Kuu chini ya Kocha huyo kutoka nchini Brazil, ikivuna alama sita, ikianza kuichapa Mbeya City 3-2 jijini Dar es salaam na kisha Dodoma Jiji FC iliyokua nyumbani.

Kocha huyo amesema bado mapema sana kwake kukiri amepata kikosi cha kwanza ambacho ataweza kukitumia mara kwa mara katika michuano ya Ligi Kuu ama ile ya Kimataifa, kutokana na kushindwa kuwatumia baadhi ya wachezaji hadi sasa.

Amesema baadhi ya wachezaji amewakuta wakiwa majeruhi na hakuwahi kuwaona wakicheza huko nyuma, hivyo inamlazimu kusubiri kuona wanavyopambana na ndipo atakuwa na jibu sahihi kuhusu kikosi cha kwanza.

“Siwezi kusema tayari nina kikosi cha kwanza, hapana, NImekuta wachezaji wengine wanaumwa mfano Phiri na tumesajili wengine wapya kama kina Baleke, hivyo nahitaji kukaa nao wote wakiwa ‘FIT’ ndipo nitapata kikosi cha kwanza.”

“Ingawa kambi ya Dubai imenipa mwanga wa timu ambayo natakiwa kuwa nayo, hii ni timu kubwa ambayo inatakiwa kuwa na malengo ya mbele.” amesema Robertinho

Wachezaji ambao ni majeruhi Simba SC ni Moses Phiri, Peter Banda na Henock Inonga Baka.

Doumbia achimba mkwara Young Africans
Mpango ataka juhudi ushughulikiaji rushwa kwenye vyombo vya haki