Klabu Simba SC ipo kwenye mahesabu makali kuhakikisha inapata ushindi mzuri kwenye michezo yao ijayo ya Ligi ya mabingwa Afrika huku Kocha Robertinho akiweka wazi mipango yake kuelekea kwenye michezo hiyo.

Kocha wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kwa sasa wachezaji wake wameonyesha wapo tayari kwa mechi kubwa za kimataifa kutokana na uwezo wanaouonyesha mazoezini na mechi mbili za kirafiki walizozicheza zimempa mwanga.

Amesema anafaham ugumu watakaoupata kutoka kwa wapinzani wao hao lakini hana hofu yoyote kutokana na maandalizi anayoendelea kuyafanya.

“Kwa sasa akili zetu zipo kwenye mchezo dhidi ya Power Dynamos, kitu kizuri kwangu ni viwango vya wachezaji wangu, wameimarika zaidi na kila mmoja anaonyesha utayari wake, ili ni jambo zuri kwangu kuelekea kwenye mchezo huu,” amesema Robertinho.

Amesema baada ya kumalizana na Wazambia hao ndipo ataanza kupanga mikakati yake kuelekea kwenye michuano ya ‘Africa Football League’ ambapo wamepangwa kucheza na mabingwa wa Misri, Al Ahly.

Vinicius Junior anajitafuta Real Madrid
Serikali kusimamia Sheria zilizopo kuwalinda Wanyama