Klabu ya Inter Milan imethibitisha kuondoka kwa meneja Roberto Mancini.

Mancini ameondoka klabuni hapo kwa kushindwa kufikia lengo la kufanya vyema msimu wa 2015/16, na tayari imearifiwa kwamba aliyekua meneja wa mabingwa wa soka nchini Uholanzi Ajax Amsterdam Frank de Boer huenda akachukua nafasi yake.

Inter Milan wamethibitisha kuondoka kwa meneja huyo kutoka nchini Italia katika ukurasa wa mtandao wa Twitter ambapo wamemshukuru Mancini kwa kazi aliyoifanya klabuni hapo tangu alipoajiriwa mwezi Novemba mwaka 2014.

Taarifa nyingine ambazo zimeriopotiwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchini Italia zinasema kwamba, matokeo ya michezo ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi, nayo yamechangia kufukuzwa kwa Mancini.

Inter Milan imepoteza michezo ya kirafiki dhidi ya Paris Saint-Germain, Bayern Munich pamoja na Tottenham.

Msimu uliopita Inter Milan ilimaliza ligi ya nchini Italia (Serie A) katika nafasi ya nne, hatua ambayo iliwakosesha nafasi ya kushirikui ligi ya mabingwa barani Ulaya.

West Ham Utd Wafanya Kweli Kwa Andre Ayew
Makonda Ashambuliwa Na Wanajangwani