Meneja wa klabu ya Inter Milan, Roberto Mancini amepanga kukinusuru kipaji cha mshambuliaji kutoka nchini Italia na klabu ya Liverpool, Super Mario Barwuah Balotelli ambaye tayari ameshatakiwa kusaka mahala pa kucheza soka lake kuanzia msimu ujao.

Tovuti ya Tuttosport imeripoti kwamba, Mancini amefikia hatua ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo kutokana na kuumizwa na mwenendo wake ambao kwa sasa unaonekana kukosa muelekeo.

Meneja huyo ambaye alimkuza na kumuendelea Balotelli, amekua akiguswa na maisha ya mshambuliaji huyo mara kwa mara, na alifikai wakati kumtamkia hatoweza kufanya nae kazi tena walipokua kwenye klabu ya Manchester City.

Taarifa hizo zimebainishwa kwamba, huenda Mancini akautaka uongozi wa Inter Milan kutuma ofa Anfield ili kumsajili Balotelli, kwa kuamini bado anaweza kumrejesha katika kiwango chake cha kupambana uwanjani.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ameonyesha kutokua tayari kufanya kazi na Balotelli baada ya kumtamkia wazi wazi kuhusu mustakabali wake klabuni hapo kwa kumwambia hana nafasi.

Balotelli, alipelekwa kwa mkopo AC Milan msimu uliopita na meneja huyo kutoka nchini Ujerumani hakubahatika kufanya nae kazi, kutokana na maamuzi ya kuondolewa Anfield kufanywa na aliyekua mkuu wa benchi la ufundi la majogoo hao Brendan Rodgers ambae miezi kadhaa iliyofuata alifutwa kazi.

FC Barcelona Waipokonya Tonge Mdomoni Real Madrid
Paul Pogba Kuvaa Jezi Namba 6 Atakapotua Man Utd