Kocha mkuu wa timu ya taifa ta Hispania Roberto Moreno amewaaga wachezaji wa timu hiyo kwa hisia kali, licha ya kumzawadia ushindi wa mabao matano kwa sifuri usiku wa kuamkia leo dhidi ya Romania.
Hispania walipata ushindi huo mnono katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2020).
Kocha Moreno aliszhindwa kujizuia na kujikuta akilia mbele ya wachezaji wake, baada ya mtanange huo uliochezwa nchini Hispania.
Moreno, aliyerithi nafasi hiyo kwa Enrique ambaye alijizulu baada ya kufiwa na mwanaye, anadaiwa uwezo wake umefika ukingoni, na tayari ameshaarifiwa na uongozi wa shirikisho la soka nchini Hispania, kusitishiwa mkataba wake.
Hatua ya kuangua kilio kwa kocha huyo ilipokelewa tofauti na wachezaji wa Hispania, ambao siku zote walimpa ushirikiano mkubwa, na kwa kudhihirisha hilo ushindi wa jana dhidi ya Romania wamemtunuku kama zawadi wa kuagana naye.
Moreno mwenye umri wa miaka 42, aliyeshinda michezo saba kati ya tisa hakuweza kuingia ndani ya ukumbi kuzungumza na vyombo vya habari licha ya kuipelea Hispania katika fainali hizo.
Tetesi zinaeleza kuwa Luis Enrique anaepewa nafasi ya kutua Emirates Stadum jijini London kwa lengo la kukinoa kikosi cha Arsenal, anapewa nafasi kubwa ya kurejea kwenye jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Hispania.