Beki wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ Andy Robertson, ameripotiwa kuingia kwenye rada za kutakiwa na Real Madrid katika dirisha hili la majira ya joto.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, nahodha huyo wa Scotland mwenye umri wa miaka 29 anatazamwa na klabu hiyo ya Ligi Kuu Hispania kama mbadala wa beki anayesumbuliwa na majeraha, Ferland Mendy.
Hata hivyo, Robertson amepewa mkataba na Liverpool hadi mwaka 2026 na hajaonyesha nia ya kuondoka.
Wakati huo huo, gazeti la Daily Mirror linaripoti Arsenal nao wanatajwa kuwa katika mpango wa kumuwani beki huyo ili kukiongezea nguvu kikois chao kwa ajili ua kuwania ubingwa msimu ujao.
Gazeti hilo pia limeitaja Real Madrid kuwa katika mchakato wa kumuwania Robertson, baada ya kuona safu yake ya ulinzi inaweza kulegalega endapo wasipoongeza mlinzi mwingine kwa ajili ya msimu ujao.
Madrid msimu huu umekuwa mbaya kwao wakiwa wametwaa taji moja tu la Copa Del Rey, huku wakishindwa kutete taji lao la Ligi Kuu lililochukuliwa na wapinzani wao, Barcelona pia akiwa bingwa mtetezi alitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali na Manchester City.