Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC huenda ikaangukia mikonini mwa klabu tatu kubwa Barani Afrika katika mchezo Robo Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba SC ilivuka hatua ya Makundi ya Michuano hiyo kwa kuifunga USGN ya Niger 4-0 jana Jumapili (April 03) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Washindi wa Kwanza kwa Kundi A, B na C ndio watakua wapinzani wa Simba SC katika hatua ya Robo Fainali.
Al Ahly Tripoli ya Libya ndio Kinara wa Kundi A, Olarndo Pirates ya Afrika Kusini wamemaliza kinara wa kundi B na Kundi C linaongozwa na TP Mazembe ya DR Congo.

Timu zilizomaliza katika nafasi ya pili kwenye kila Kundi ikiwemo Simba SC, zitaanzia nyumbani kucheza Robo Fainali ya Mkondo wa Kwanza kisha itamalizia Ugenini Kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili.

Michezo ya Mkondo wa kwanza imepangwa kuchezwa kati ya April 15-17, huku Michezo ya Mkondo wa pili ikitarajiwa kuchezwa kati ya April 22-24.

Hafla ya Kupanga michezo ya Hatua ya Robo Fainali inatarajiwa kufanyika Kesho Jumanne (April 05) Mjini Cairo nchini Misri saa kumi jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Adebayor: Sikuwa na Presha yoyote, Simba ni kubwa Afrika
Will Smith anakiona cha mtemakuni kisa Kofi