Aliyekua mshambuliaji klabu za Manchester City, Real Madrid na AC Millan Robson de Souza (Robinho), amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya tukio la ubakaji mwaka 2013.

Robinho amekutwa na hatia hiyo, akidaiwa alifanya tukio hilo mjini  Milanese nchini Italia ambapo alimbaka binti mwenye umri wa miaka 23 na kisha kumtelekeza.

Inadawai kipindi wakati Robinho akitekeleza ubakaji huo alikuwa akiichezea klabu ya Ac Millan na huko ndiko alikofanikiwa kumfahamu binti huyo Mualbania kabla ya kumfanyia kitendo hicho.

Robinho kwa sasa anacheza soka nchini kwao Brazil katika Klabu ya Atletico Mineiro na amepewa muda na mahakama ya nchini Italia kukata rufaa kama anaona anapaswa kufanga hivyo kabla ya hukumu kuanza.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Robinho kupatwa na kesi ya ubakaji kwani mwaka 2009 mshambuliaji huyo alikumbwa na kashfa kama hiyo baada ya kudaiwa kumbaka mwanafunzi wa Chuo cha Leeds nchini Uingereza.

Mwanariadha mlemavu aongezewa kifungo jela
Kingue aongozewa mwaka mmoja Azam FC