James Rodriguez alifunga bao lake la kwanza akiwa Bayern Munich katika mchezo wa ligi ya Bundesliga ambao klabu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya FC Schalke 04.

Bao la Rodriguez, ambaye yuko Bayern Munich kwa mkono akitoka Real Madrid ya Hispania lilikuwa bao la pili katika mchezo huo baada ya Robert Lewandowski kutangulia kufunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 25.

Kipindi cha pili Rodriguez alitoa pasi iliyozaa goli la tatu baada ya kuwatoka mabeki wawili wa Schalke 04 nakumpa pasi nzuri Arturo Vidal aliyepachika mpira wavuni dakika ya nakuwafanya vijana wa Carlo Ancelotti kuibukaa na ushindi wa mabao 3-0.

Michezo mingine ya Bundeslaga iliyopigwa Borussia Monchengladbach walilaza Stuttgart 2-0 wakati Augsburg wakiendelea na mwanzo wao mzuri baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya RB Leipzig waliomaliza wa pili msimu uliopita kwa bao la Michael Gregoritsch.

Rodriguez alisajiliwa na Real Madrid kwa pauni milioni 71 kutoka Monaco mwaka 2014

Wolfsburg walitoka sare ya 1-1 na Werder Bremen huku mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi ambaye yuko kwa mkopo Wolfsburg aliwafungia bao lake la kwanza.

 

 

 

 

Video: JPM aagiza kujengwa uzio kulizunguka eneo la Mererani
Uuzaji wa pombe siku za wiki wapigwa vita