Wanamgambo wa Kipalestina wanasema wamerusha makombora 130 katika mji wa Israeli wa Tel Aviv baada ya shambulio la anga la Israeli kuangusha ghorofa katika eneo la ukanda wa Gaza.

Jumba hilo la ghorofa 13 lilishambuliwa saa moja unusu baada ya wakazi na wenyeji wa eneo hilo kushauriwa waondoke, shirika la habari la Reuters liliripoti.

Jeshi la Israel linasema kuwa linalenga wanamgambo mjini Gaza kujibu shambulio la awali la roketi.

Watu 31 wameuawa baadhi yao katika ghasia mbaya zaidi zilizowahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Jamii ya kimataifa imetoa wito kwa pande zote mbili kukomesha mapigano, yaliyofuatiwa na siku kadhaa za ghasia mjini Jerusalem.

Siku chache zilizopita zimekumbwa na ghasia mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa mjini Jerusalem tangu mwaka 2017.

Miradi ya maji kukamilika ifikapo 2025
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 12, 2021