Hofu imetanda juu ya moyo wa ‘Ninja’ kutoka Tanga, Roma Mkatoliki masaa machache baada ya kuachia wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Viva’.

Rapa huyo anahofia wimbo wake kufungiwa muda wowote kwa madai kuwa ameanza kupokea taarifa za kufungiwa wimbo huo ambao umerusha makombora mazito yanayogusa sehemu ambazo zimewafanya hata mashabiki wake kuhofia hatma ya wimbo huo.

Akiongea na Jabir Saleh katika kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm jana usiku, Roma alisema kuwa sio mara ya kwanza watu kuhofia kupokea nyimbo zake kutokana na mashairi mazito anayoyaandika. “Hakuna aliyenituma, nimetumwa na wananchi niwaongelee na nilichoongea ni ukweli mtupu,” alisema Roma huku akitetea baadhi ya mitari tata iliyoko kwenye wimbo huo.

Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi, mashabiki wake walikuwa wanasubiri kwa hamu kusikia anasema kitu kuhusu kile kinachoendelea hivyo alitumia muda mwingi kuandika kile alichokiita ukweli mtupu.

Akielezea nini kitatokea endapo wimbo wake utafungiwa, Roma alisema kuwa ingawa uamuzi huo utaathiri harakati zake lakini anaamini ujumbe wake utafika.

“Hata wakati ule nilipotoa wimbo wa Mr. President, kuna baadhi ya radio ulikuwa ukienda unakuta kabisa ‘memo’ kuwa wimbo huo usichezwe kabisa. Lakini wimbo ulihit mitaani tu hivyo hivyo,” alisema.

Alieleza kuwa wimbo wake wa Mathematics ulifanya vizuri zaidi ya nyimbo zake zote zilizopita kwa sababu tu uliruhusiwa kuchezwa radioni bila vipingamizi na sio kwamba ndio ulikuwa wimbo mkubwa zaidi.

Usikilize hapa:

Prince Ali Atangaza Kurejea FIFA
Twiga Stars Yashindwa Congo Brazzaville