Roma Mkatoliki amesema watu wengi wamejitokeza kutaka kulipia gharama za utayarishaji wa video ya wimbo wake wa ‘Viva’ uliotoka wiki chache zilizopita.

Amesema kuwa baada ya kuachia wimbo huo, hakuwa na mpango wa kufanya video lakini changamoto zilizojitokeza baada ya radio kadhaa kukataa kuucheza wimbo huo zimemfanya afikirie kufanya video ili kuupa uhai zaidi.

“Kiukweli mwanzo sikupanga kufanya video yake lakini baada ya kuona imekosa airtime ya kutosha kwenye redio nimeshauriwa kufanya video. Kuna watu wengi tayari wameshasema watalipia gharama ya video ya Viva, kwahiyo sasa hivi nipo kwenye maandalizi ya mwisho,” aliuambia mtandao wa Bongo5.

Rapa huyo mwenye mistari tata alifafanua kuwa bado hajapata taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka husika kuwa wimbo wake huo umefungiwa lakini amekuwa akielezwa na watangazaji wa baadhi ya radio kuwa wimbo wake umezuiwa kuchezwa katika vituo vyao.

2Face Awasilisha Ombi Maalum Kwa Dbanj Na Donjazzy
CCM Yalalamikia Matokeo Ya Utafiti Wa Twaweza