Hatimaye, Roma Mkatoliki ataika kiu ya mashabiki wake waliokuwa wakisubiri kuisikia ngoma yake mpya aliyoibatiza ‘Kaa Tayari’ itakayotoka Kesho (Jumatano, Julai 13).

Katika Kaa Tayari, Roma amewashirikisha Jos Mtambo na Darassa, huku midundo ikinyongwa na J-Ryder.

Roma ambaye amekuwa akitoa nyimbo chache zinazodumu kwa muda mrefu na kutengeneza mada na mijadala mingi mitaani na kwenye mitandao ya kijamii, amewataka mashabiki wake kuiweka katika kumbukumbu nzuri siku ya kesho.

“Saa #8:01 Nitaachia Audio!! Na Saa #9:01 Nitaachia Video,” amesema Roma.

 

Hivi karibuni, Roma aliiambia Dar24 kuwa wimbo huo uliopikwa ndani ya Tongwe Records na video yake kuongozwa na Nick Dizzo itakuwa ‘surprise’ nzuri kwa mashabiki wake.

“Msanii mzuri ni yule ambaye anafanya kitu ambacho watu hawaexpect. Kwahiyo wakati mwingine unaweza kuachia jiwe ambalo watu hawalitegemei. Ndio maana kwenye ‘Kaa Tayari’ tukawaambia ‘hapana ili iwe exclusive inabidi wasubiri wasikilize Roma ameimba nini,” Roma aliiambia Dar24.

Kesho ndio siku ya kumtoa huyo mwali, endelea kutembelea Dar24 kusikiliza na kuona ‘Kaa Tayari’. Tunza hiyo tarehe.

Video: Rais Magufuli Azizungumzia Hizi Taarifa Zilizosambaa kuhusu Mkurugenzi Aliyemteuwa
Brazil Yapata Pigo Kuelelea Michuano Ya Olimpiki