Rapa Roma Mkatoliki ambaye wengi walimfahamu kutokana na namna alivyoweza kuitengeneza mistari mikali inayobeba matukio ya siasa nchini, amewataka mashabiki wake kutambua kuwa suala la siasa sio la msimu.

Rapa huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo na video ya wimbo wake ‘Kaa Tayari’, amesema kuwa siasa ni maisha ya wananchi ya kila siku na kila wanachokifanya hutokana na siasa.

“Unajua nikutafsirie kwa kifupi tu kuwa siasa ni kila kitu. Yaani ukiamka asubuhi ukanywa chai, ile sukari unayokoroga imetokana na siasa. Ukianza movement zako ukapanda daladala au lile gari la mwendo kasi ni siasa,” Roma aliiambia XXL ya Clouds Fm.

“Tusichukulie kama siasa ni kitu kinachotokea kila baada ya miaka mitano kama kombe la dunia kila baada ya miaka minne. Siasa ni maisha yetu tunayoishi kila siku,” Roma anakaririwa.

Alisema kuwa bado anayo mengi ya kuimba katika maisha ya siasa kwakuwa bado yapo mengi ya kupongeza na ya kukosoa.

Serikali ya Kenya yamtimua Koffi Olomide Kwa kumpiga mnenguaji wake wa kike
Kikwete awashtaki CCM kwa Magufuli, amtaka ashughulikie haya