Mmiliki wa Klabu Bingwa Duniani Chelsea FC, Roman Abramovich ametangaza kujiuzulu ndani ya klabu hiyo ya jijini London.

Kujiuzulu kwake kunamaanisha amejitoa kwenye uongozi wa bodi ya klabu, hivyo hatokuwa mtu wa mwisho kutoa tamko na maamuzi kama ilivyokuwa hapo kabla.

Badala yake majukumu hayo ameyaacha kwenye uongozi wa bodi ambao unaongozwa na mwanamama, Marina Granovskaia pamoja na Rais wa Chelsea, Bruce Buck.

Kujiuzulu kwa Abramovich hakuna maana kwamba ameiuza klabu au amejitoa kabisa hatohusika tena, badala yake anabaki kuwa mmiliki wa klabu lakini  hatokuwa na sauti ya mwisho kwenye kufanya maamuzi.

Kwa lugha rahisi anaendelea kuwa mmiliki lakini majukumu yanaamuliwa na kundi la viongozi wa bodi.

Shinikizo laongezeka kwa Urusi
Pablo Martin: Tunakwenda kuishangaza Afrika