Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil na bingwa wa kombe la dunia mwaka 1994 Romário de Souza Faria ameweka bayana mipango yake ya kuwania urais wa shirikisho la soka nchini humo CBF kwa lengo la kulikwamua soka la Brazil kuondokana na kashfa za rushwa.

Romario mwenye umri wa miaka 51 ambaye kwasasa ni seneta Rio de Janeiro anaongoza kamati huru ya kuchunguza masuala ya rushwa yanayoliandama soka la Brazil na ametangaza nia ya kugombea kiti hicho ikiwa ni siku nne baada ya FIFA kumsimamisha kwa siku 90 Rais wa sasa wa CBF Marco Polo del Nero.

Romario ambaye ni miongoni mwa wanasiasa maarufu nchini Brazil, amejisifu kuwa yeye ni chaguo sahihi kwa nafasi hiyo ya urais na anaamini ataivusha Brazil kutoka hapo ilipo sasa.

Aliwahi kufunga magoli matano kwenye kombe la dunia mwaka 1994 nchini Marekani wakati Brazil ikitawazwa kuwa mabingwa na kabla ya kustaafu mwaka 2009 aliweka rekodi ya kufunga zaidi ya magoli 1000 akiwa na timu mbalimbali ikiwemo FC Barcelona.

Tanzania yazidi kuporomoka viwango vya soka
Marion Bartoli atengua maamuzi