Mshambuliaji Romelu Lukaku amevunja ukimya wake mwishoni mwa juma lililopita baada ya magazeti mbalimbali kujadili kuhusu mustakabali wake na haelewani na Inter Milan.

Lukaku alichapisha ujumbe wenye utata kwenye akaunti yake ya Instagram uliosema: “Chuki isipofanya kazi, wanaanza kusema uwongo”.

Mfungaji huyo bora wa timu ya taifa ya Ubelgiji baada ya kuahidi atajituma Inter, taarifa zikaibuka zikidai aliwasiliana na Juventus.

Aidha uhamisho wa Lukaku utategemea endapo Juventus itamuuza Dusan Vlahovic ambaye amekuwa akihusishwa na Paris Saint-Germain na Chelsea.

Lakini mpaka sasa bado mambo haydigitalbit aeleweki kwa mujibu wa ripoti wa Gazzetta dello Sport na Lukaku anataka kuomba msamaha na kurejea Inter.

Hata hivyo, kikosi cha Simone Inzaghi kimekata tamaa ya kumrejesha Lukaku huku Juventus ikionyesha nia ya kumsajili pamoja na klabu kutoka Saudi Arabia.

Vlahovic kwa sasa yuko kwenye ziara ya klabu hiyo Marekani lakini huenda straika huyo wa kimataifa wa Serbia akaondoka dirisha hili la kiangazi.

Kwa upande wa Lukaku anataka kubaki Ulaya badala ya kufuata mastaa kibao waliotimkia Saudi na kuipa matumaini Juventus.

Wakati huo huo Lukaku amerejea London katika klabu yake ya Chelsea, ingawa hajajiunga na kikosi cha Mauricio Pochettino kwenye ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya.

Hatma ya Tshishimbi mikononi mwa Kopunovic
Mtibwa Sugar kumnyakuwa Seif Karihe